Katika maisha yetu ya kimwili na ya kiroho, daima kuna majaribu na vikwazo vingi. Zamani, Waisraeli walipokabiliwa na majaribu makubwa—jangwa lisilo na maji wala chakula na nchi ya Kanaani iliyokaliwa na majitu, Yoshua na Kalebu waliweka tumaini lao katika Mungu pekee. Kama wao, tunahitaji imani kuona mlango wa tumaini ambao Mungu Ametufungulia katikati ya magumu.
Kama vile kwa njia ya ufufuo na kupaa kwa Yesu, Mungu Alifungua mlango wa tumaini kwa ufalme wa mbinguni kwa watakatifu wa Kanisa la mapema waliokata tamaa kwa kusulubiwa kwa Yesu, na kama vile Yesu Alivyomwonyesha Petro, ambaye hakuvua kitu usiku kucha, muujiza unaotokea tunapotenda kulingana na neno Lake, leo, pia, maneno ya Kristo Ahnsahnghong, “Injili itahubiriwa ulimwenguni kote,” hakika yatatimizwa.
“Ee BWANA, nijulishe mwisho wa maisha yangu na hesabu ya siku zangu; nijalie kujua jinsi maisha yangu yanavyopita upesi. “Lakini sasa Bwana, nitafute nini? Tumaini langu ni kwako. Zaburi 39:4–7
… lakini yule atakayevumilia hadi mwisho ataokolewa. Injili ya Ufalme itahubiriwa ulimwenguni kote kuwa ushuhuda kwa mataifa yote. Ndipo mwisho utakapokuja. Mathayo 24:13–14
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha