Mfalme Asa na Mfalme Yehoshafati walizishika kwa uaminifu amri na sheria za Mungu, wakabomoa kila sanamu, na wakawaongoza watu pamoja na ufalme wao wakiwa na imani isiyotikisika kwamba mradi tu Mungu yuko pamoja nao, kila jambo lingekwenda vizuri. Kwa sababu hiyo, Mungu Akaipa nchi yao amani, na Akawajaza baraka nyingi pamoja na heshima na utukufu.
Kupitia historia iliyoandikwa katika Biblia, Mungu Amewaonyesha wanadamu njia ya kupokea baraka zake. Hatupaswi kufanya kosa la Mfalme Asa la miaka yake ya mwisho, ambapo alitegemea mataifa yenye nguvu badala ya kumtafuta Mungu. Wala tusifanye kama Mfalme Yehoshafati, aliyejiunga na watu waovu na kushirikiana nao katika mipango yao. Kwa sababu tunapomsahau Mungu na kuweka tumaini letu kwa watu au mazingira yanayotuzunguka, Mungu huondoa baraka Zake kutoka kwetu.
Basi wakakusanyika huko Yerusalemu mwezi wa tatu katika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Asa. Wakati huo wakamtolea BWANA dhabihu za ngʼombe 700, kondoo na mbuzi 7,000 kutoka zile nyara walizoteka. Wakafanya agano kumtafuta BWANA, Mungu wa baba zao kwa moyo wao wote na kwa roho yao yote. . . . Yuda wote wakafurahia kile kiapo kwa sababu walikuwa wameapa kwa moyo wao wote. Wakamtafuta Mungu kwa bidii, naye akaonekana kwao. Kwa hiyo BWANA akawastarehesha pande zote. 2 Nyakati 15:10–15
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha