Tunapoangalia nuru, kivuli kinatokea nyuma yetu, lakini tunapoipa mgongo nuru, kivuli huzuia njia yetu.
Vivyo hivyo, wanadamu wanapoenda kumwelekea Mungu ambaye ni nuru, giza haliwezi kamwe kuwazuia.
Kama Yeremia katika enzi ya Baba na mitume katika enzi ya Mwana, tunapowasilisha nuru ya utukufu wa Mungu, tunaweza kukabili mateso na vizuizi karibu nasi.
Walakini, mwishowe, tutapokea baraka nyingi.
Isaya, Yeremia, na Ezekieli waliwasilisha nuru ya Mungu Yehova katika enzi ya Baba, na Mitume Paulo, Petro, na Yohana waliwasilisha nuru ya utukufu wa Yesu katika enzi ya Mwana.
Vivyo hivyo, katika enzi ya Roho Mtakatifu, waumini wa Kanisa la Mungu katika nchi 175 duniani kote wanaiwasilisha nuru ya utukufu ya Kristo Ahnsahnghong na Yerusalemu Mama wa Mbinguni Waliokuja kama Waokozi.
“Ondoka, angaza, kwa kuwa nuru yako imekuja na utukufu wa BWANA umezuka juu yako.
Tazama, giza litaifunika dunia na giza kuu litayafunika mataifa, lakini BWANA atazuka juu yako na utukufu wake utaonekana juu yako.
Mataifa watakuja kwenye nuru yako na wafalme kwa mwanga wa mapambazuko yako.
Isaya 60:1–3
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha