Tunaweza kuona nguvu ya neno la Mungu pale Adamu na Eva walipokufa kwa kula matunda ya mti wa kujua mema na mabaya; yule mnyang’anyi kwenye upande wa kuume wa msalaba alipookolewa; wale vipofu wawili walipoponywa; yule mwanamke aliyekuwa na tatizo la kutokwa na damu kwa muda wa miaka kumi na miwili alipoponywa; na kupitia ukweli kwamba yeyote aulaye mwili wa Yesu na kuinywa damu Yake kwa kushiriki mkate na divai ya Pasaka atapokea zawadi ya uzima wa milele.
Katika enzi ya Mwana, Yesu pekee ndiye Aliyewapa maji ya uzima wale waliomjia katika Siku ya Mwisho na Iliyo Kuu ya Sikukuu ya Vibanda.
Katika enzi ya Roho Mtakatifu, wale wanaokuja kwa Kristo Ahnsahnghong na Mungu Mama, ambao Walikuja kama Roho na Bibi arusi, watapokea maji ya uzima, yaani Roho Mtakatifu. Hao ndio wanaoweza kutimiza mambo yote kwa nguvu ya neno la Mungu.
Siku ile ya mwisho ya Sikukuu, siku ile kuu, wakati Yesu akiwa amesimama huko, akapaza sauti yake akasema, “Kama mtu yeyote anaona kiu na aje kwangu anywe. Yeyote aniaminiye mimi, kama Maandiko yasemavyo, vijito vya maji ya uzima vitatiririka ndani mwake.” Yesu aliposema haya alimaanisha Roho Mtakatifu ambaye wote waliomwamini wangempokea, . . .
Yohana 7:37–39
Roho na bibi arusi wanasema, “Njoo!” Naye asikiaye na aseme, “Njoo!” Yeyote mwenye kiu na aje, na kila anayetaka na anywe maji ya uzima bure.
Ufunuo 22:17
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha