Mungu Alimwamuru Mose kujenga hema ili kuweka amri kumi za pili ndani yake. Watu walipotambua dhambi yao iliyosababisha kuvunjwa kwa Amri Kumi za kwanza, walitubu na kwa hiari wakaleta vifaa kwa ajili ya hema. Hii ikawa chimbuko la Sikukuu ya Vibanda.
Baada ya hapo, walijenga vibanda katika ua wa hekalu au juu ya paa la hekalu kwa kutumia aina zote za matawi ya miti.
Sikukuu ya Vibanda ni siku ambayo Kristo Ahnsahnghong na Mungu Mama hukusanya watu Wao wote pamoja. Wanadamu lazima wamshukuru Mungu ambaye Amewasamehe na kuwaokoa kutoka dhambi zao. Na kupitia Roho Mtakatifu wa mvua ya mwisho waliyopokea, lazima wapate wanafamilia wote wa mbinguni ulimwenguni kote ambao ni vifaa vya Hekalu la mbinguni la Yerusalemu.
Kwa hiyo hili ndilo asemalo BWANA Mungu Mwenye Nguvu Zote: “. . . nitayafanya maneno yangu vinywani mwenu kuwa moto, na watu hawa wawe kuni zinazoliwa na huo moto.
Yeremia 5:14
Ndani yake jengo lote limeshikamanishwa pamoja na kusimamishwa ili kuwa Hekalu takatifu katika Bwana. Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja ili mpate kuwa makao ambayo Mungu anaishi ndani yake kwa njia ya Roho wake.
Waefeso 2:21–22
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha