Sababu ‘wadudu siku-moja’ huishi tu kwa siku moja, mbwa huishi miaka 15, na binadamu huishi miaka 100 ni kwa sababu wanarithi maisha hayo kutoka kwa mama zao. Wanadamu wote wanaweza kuwa “watoto wa ahadi” ambao wanapokea uzima wa milele kutoka kwa Mungu iwapo tu wanakutana na Mungu Mama ambaye Anao uzima wa milele.
Biblia inatufundisha kuhusu familia ya Mbinguni kupitia mfumo wa familia ya duniani ambao ni kivuli, na kuhusu Baba wa Mbinguni na Mama wa Mbinguni kupitia Adamu na Eva na Mwana-Kondoo na Mke Wake (Bibi arusi). Pia Biblia inatufundisha kwamba ni Mungu Mama tu, ambaye Anafananishwa na Yerusalemu, ambaye Anao Uzima wa milele.
Hii ndiyo ahadi yake kwetu, yaani, uzima wa milele.
1 Yohana 2:25
Naye akanichukua katika Roho hadi kwenye mlima mkubwa na mrefu, akanionyesha ule Mji Mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu.
Ufunuo 21:10
Lakini Yerusalemu wa juu ni huru, nayo ndiye mama yetu. . . . Basi, sisi ndugu zangu, ni kama Isaki, tu watoto wa ahadi.
Wagalatia 4: 26–28
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha