Mungu Aliiamuru siku ambayo Mose alishuka akiwa na seti ya pili ya Amri Kumi kuwa Siku ya Upatanisho, na Sikukuu ya Vibanda ilikuwa sikukuu ambapo Waisraeli walijenga hema ili kuweka vile vibao vya mawe vya Amri Kumi.
Kama tulivyoona miaka 3,500 iliyopita, kipengele muhimu zaidi cha kujenga hekalu la Mungu ni kuwa na moyo ambao ulisukumwa kujiunga na kuwa na moyo wa kupenda kushiriki.
Watu kama hao walitoa vifaa tele kwa ajili ya ujenzi wa hekalu.
Leo, ulimwengu mzima unakusanyika kwa Kristo Ahnsahnghong na Mama wa Mbinguni Yerusalemu kwa sababu watu wa Mungu wanafananishwa na vifaa mbalimbali vinavyounda Hekalu la Yerusalemu.
Kuna unabii kwamba, kama vile matawi mbalimbali yalivyokusanywa kwa ajili ya Sikukuu ya Vibanda katika Agano la Kale, watu wa Mungu watakusanyika pamoja kama aina mbalimbali za miti kwa Yerusalemu.
[N]a kila mmoja aliyependa na ambaye moyo wake ulimsukuma alikuja na kuleta sadaka kwa BWANA, kwa ajili ya kazi katika Hema la Kukutania, kwa ajili ya huduma yake yote na kwa ajili ya mavazi matakatifu.
Wote waliokuwa na utayari, wanaume kwa wanawake, wakaja . . .
Kutoka 35:21–22
Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ndiye jiwe kuu la pembeni.
Ndani yake jengo lote limeshikamanishwa pamoja na kusimamishwa ili kuwa Hekalu takatifu katika Bwana.
Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja ili mpate kuwa makao ambayo Mungu anaishi ndani yake kwa njia ya Roho wake.
Waefeso 2:20–22
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha