Kama msemo unavyosema, “Ziwa la dhahabu katika mchanga wa jangwa ni la thamani ndogo kuliko chemchemi safi, baridi na kwa kondoo mmoja aliyepotea, mvulana mchungaji ni mkuu kuliko mfalme tajiri sana,” kile kilicho cha thamani duniani na kile kilicho cha thamani katika ufalme wa mbinguni ni tofauti kabisa. Utajiri, heshima, na mamlaka ambavyo watu wengi ulimwenguni huthamini havina thamani katika ufalme wa mbinguni. Ndiyo maana watakatifu wa Kanisa la mapema waliishi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni hata katikati ya mateso.
Katika ufalme wa Mungu, kazi yenye thamani zaidi ni kutenda kulingana na neno la Mungu. Waumini wa Kanisa la Mungu hutafuta hata nafsi moja aliyepotea kwa ukweli wa agano jipya, wakiamini neno la Mungu kwamba watatawala kama wafalme katika ufalme wa mbinguni na kung’aa kama nyota milele na milele.
Watu hawa wote wakafa katika imani bila kuzipokea zile ahadi, lakini waliziona kwa mbali na kuzishangilia. Nao walikubali kwamba walikuwa wageni na wasiokuwa na maskani hapa duniani. Waebrania 11:13
Wale wenye hekima watangʼaa kama mwanga wa mbingu, nao wale ambao huwaongoza wengi kutenda haki, watangʼaa kama nyota milele na milele. Danieli 12:3
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha