Miaka elfu mbili iliyopita, Mungu Muumba Alikuja duniani kwa jina la Yesu, na Akaanzisha Agano Jipya. Kupitia Agano Jipya, watoto wa Mungu, ambao wanateseka kutokana na dhambi na mauti, wanaweza kupata msamaha wa dhambi na uzima wa milele. Kwa miaka mitatu, Yesu Aliwawekea wanafunzi Wake kielelezo cha kushika Agano Jipya.
“Mimi nimewawekea kielelezo kwamba imewapasa kutenda kama vile nilivyowatendea ninyi.” Yohana 13:15
Baada ya Ufufuo, Yesu Aliwaomba wanafunzi Wake wafundishe watu wote kushika Agano Jipya ili kwamba waweze kuokolewa. (Mathayo 28:19)
Wakifuata maneno ya Yesu, wanafunzi Wake walihubiri Agano Jipya. Katika Agano Jipya, ambalo kupitia hilo tunaweza kuwa na msamaha wa dhambi, kuna agizo kwa ajili ya ibada. Mwanaume akifunika kichwa chake wakati wa ibada, ni aibu kwa Mungu; mwanamke asipofunika kichwa chake, ni aibu kwa kichwa chake. (1 Wakorintho 11:4)
Katika kanisa linalofuata Agano Jipya ambalo lilianzishwa na Kristo, mwanamke anafunika kichwa chake kwa uatji wakati wa ibada, na mwanaume hafuniki kichwa chake. Walakini, baada ya kupaa kwa Yesu, baadhi ya wanawake walisisitiza kwamba haikuwapasa kuvaa utaji.
Kwa sababu ya hili, Mtume Paulo aliwahimiza kuvaa utaji, akielezea kwamba nywele ndefu inapendeza kwa mwanamke kwa maumbile ya asili ya kibinadamu.
“Hukumuni ninyi wenyewe: Je, inafaa kwa mwanamke kumwomba Mungu bila kufunika kichwa chake? Je, maumbile ya asili hayatufundishi kuwa ni aibu kwa mwanaume kuwa na nywele ndefu? Lakini mwanamke akiwa na nywele ndefu ni utukufu kwake? Kwa maana mwanamke amepewa nywele ndefu ili kumfunika. Kama mtu anataka kubishana juu ya jambo hili, sisi wala makanisa ya Mungu hatutambui desturi nyingine.” 1 Wakorintho 11:13-16
Biblia inasema dhahiri kwamba mwanamke anapaswa kufunika kichwa chake kwa utaji wakati wa ibada. Desturi ya kuvaa utaji kwa mwanamke wakati wa ibada ni mojawapo ya maagizo ya Agano Jipya ambayo Yesu Alifundisha na Mtume Paulo alihubiri.
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha