Siku ya Upatanisho ni siku kuu ambapo dhambi zote za watu na makuhani zinasamehewa. Waisraeli walisahau neema ya Mungu na wakatenda dhambi kwa kuabudu sanamu, ndama wa dhahabu. Ndiyo maana Mose alivunja seti ya kwanza ya Amri Kumi zilizotolewa na Mungu. Waisraeli walitubu dhambi zao na Mungu Akawapa seti ya pili ya Amri Kumi; siku hii ikawa asili ya Siku ya Upatanisho.
Katika Agano la Kale, dhambi zote za Israeli zilihamishiwa patakatifu kwa muda hadi Siku ya Upatanisho. Leo, dhambi zetu zote zimehamishiwa kwa Kristo Ahnsahnghong na Mungu Mama, ambao ni uhalisi wa patakatifu. Basi, katika Siku ya Upatanisho, dhambi zetu zote zinahamishiwa kwa Shetani, ambaye ndiye mwanzilishi wa dhambi. Hatimaye, Shetani atahukumiwa kuzimu, yaani, jehanamu, na wakati huo, dhambi zote hatimaye zitatoweka.
BWANA akamwambia Mose, “Siku ya kumi ya mwezi huu wa saba ni Siku ya Upatanisho. Mtafanya kusanyiko takatifu, mfunge, nanyi mtoe sadaka kwa BWANA ya kuteketezwa kwa moto.”
Walawi 23:26–27
Siku iliyofuata, Yohana alimwona Yesu akimjia akasema, “Tazama, Mwana- Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu!
Yohana 1:29
Naye ibilisi aliyewadanganya akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti walikokuwa wametupwa yule mnyama na yule nabii wa uongo. Watateswa humo usiku na mchana, milele na milele.
Ufunuo 20:10
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha