Samoni huishi baharini na kisha hurudi mahali pao pa kuzaliwa ili kutaga mayai. Katika mchakato huo, kama vile samoni huvumilia maumivu kwa kutumia nishati yake iliyohifadhiwa bila kula, sisi pia, lazima tuyashinde maumivu ya kuzaliwa upya kwa kutupilia mbali tabia na mwenendo wote mbaya tuliojifunza katika ulimwengu huu na kujitahidi kurudi nyumbani kwetu pa milele ya mbinguni ambapo Baba na Mama hukaa.
Wakati huu, mataifa yote yanapokimbilia mikononi mwa Yerusalemu Mama wa Mbinguni kama ilivyotabiriwa katika Biblia, waumini wa Kanisa la Mungu daima hutekeleza “Maneno ya Upendo wa Mama” kulingana na mafundisho Yake, wakifunua utukufu wa Yerusalemu Mama wa Mbinguni kwa ulimwengu mzima kupitia matendo yao mema.
Msifuatishe tena mfano wa ulimwengu huu, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu. Ndipo mtaweza kujaribu ili kuthibitisha mapenzi ya Mungu yaliyo mema, yanayopendeza na kamilifu machoni pake. Warumi 12:2
“Ondoka, angaza, kwa kuwa nuru yako imekuja na utukufu wa BWANA umezuka juu yako. Tazama, giza litaifunika dunia, na giza nene litayafunika mataifa, lakini BWANA atazuka juu yako na utukufu wake utaonekana juu yako. Mataifa watakuja kwenye nuru yako na wafalme kwa mwanga wa mapambazuko yako. Isaya 60:1–3
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha