Makanisa mengi ulimwenguni yanasisitiza kwamba siku ya Sabato imeondolewa kwa sababu ni sehemu ya sheria ya Agano la Kale.
Hata hivyo, kama watu wa Mungu, tumeitwa kuzishika Amri Kumi zote—kuanzia amri ya kwanza hadi ya kumi, hakuna hata amri moja tunayoweza kuipuuza. Hakuna anayeweza kusema kwa usahihi, “Amri tisa kati ya Amri Kumi lazima zishikwe, lakini amri ya nne haihitaji kushikwa.”
Hata makanisa ambayo hayashiki siku ya Sabato yanathibitisha wazi umuhimu wa Amri Kumi.
Kwa hiyo, dai kwamba “siku ya Sabato haihitaji kushikwa kwa sababu iliondolewa kama sehemu ya sheria ya Agano la Kale” linajipinga na ni la uongo. Hata leo, tunapaswa kuitakasa siku ya Sabato, kama vile amri ya nne inavyoagiza.
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha