Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu inajumuisha roho ya dhabihu, kujitoa, na upendo wa Kristo Aliyejidhabihu Mwenyewe ili kuwaokoa wanadamu waliotenda dhambi mbinguni.
Tunapaswa kuiadhimisha Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, kwa nia ya kutubu dhambi zetu kwa njia ya usulubisho na maisha ya Kristo, na kushiriki kwa shangwe katika mateso Yake.
Mungu Alikuja hapa duniani kwa ajili ya wokovu wa wanadamu, ila hata Petro, aliyejulikana kwa imani yake, Yuda Iskariote, na wanafunzi wengine wote walitenda matendo ya kuhuzunisha machoni pa Mungu.
Tukijifunza kutoka kwa upendo wa Mungu, ambaye hakuwadharau wenye dhambi kama hao bali aliwahurumia, sasa ni lazima tutembee njia ya imani tukichukua msalaba wetu wenyewe.
“Lakini haya yote yametukia ili maandiko ya manabii yapate kutimia.” Ndipo wanafunzi wake wote wakamwacha na kukimbia.
Mathayo 26:56
Ndipo Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Mtu yeyote akitaka kunifuata, ni lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake, anifuate.”
Mathayo 16:24
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha