Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu ni sikukuu kwa ajili yetu kutazama nyuma juu ya maisha na mateso ya Kristo, kutubu dhambi zetu, na kuacha nyuma imani ya kitoto. Kama Paulo, imani yetu inapasa kukua na kuwa imani iliyokomaa, ili kwamba tuweze kujifunza jinsi ya kuwa na shukrani ya kweli kwa ajili ya magumu mengi tunayokabili katika maisha yetu ya imani.
Jambo Muhimu la Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu ni Kutambua Maana ya Dhabihu ya Kristo na Mateso Msalabani. Yesu hakuishi maisha ya utukufu wala ya heshima ambayo Anastahili kama Mungu. Alivumilia mateso ya msalaba kwa ajili ya watoto Wake pamoja na dhihaka na chuki kutoka kwa wengine. Hali kadhalika, waumini wa Kanisa la Mungu huishi maisha yao kwa ajili ya wengine, na si kwa ajili ya furaha yao wenyewe. Wanajitahidi kuzaliwa upya kama viumbe kamili ambao Mungu Anapendezwa nao.
Ndipo kuhani mkuu akararua mavazi yake na kusema, “Amekufuru! Tuna haja gani tena ya mashahidi zaidi? Tazama, sasa ninyi mmesikia hayo makufuru. Uamuzi wenu ni gani?” Wakajibu, “Anastahili kufa,” Kisha wakamtemea mate usoni na wengine wakampiga ngumi. Wengine wakampiga makofi na kusema, “Tutabirie, wewe Kristo! Ni nani aliyekupiga?”
Mathayo 26:65–68
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha