Dhabihu za Agano la Kale zina toba ya wenye dhambi
na upatanisho wa Mungu. Baada ya Adamu na Eva kutenda dhambi ya kwanza,
Mungu Aliwaruhusu Kaini na Abeli kutoa dhabihu
ambayo kupitia hiyo waliweza kuuendea mti wa uzima tena.
Dhabihu ziliendelea katika wakati wa Mose
nazo zikabadilika kuwa ibada katika nyakati za Agano Jipya.
Bila ibada tunazozitoa kwa Mungu,
msamaha wa dhambi hauwezi kupewa kwetu.
Katika ibada zote za Agano la Kale,
wanyama walimwaga damu kwa niaba ya wenye dhambi.
Walakini, katika nyakati za Agano Jipya,
Yesu Kristo Mwenyewe Alitolewa dhabihu kama sadaka ya dhambi.
Kwa hiyo, lazima tushike ibada zote
ambazo Yesu Alianzisha kwa njia ya dhabihu Yake, katika roho na kweli.
Ukweli kwamba Yesu Alikuwa kuhani mkuu
unamaanisha kwamba lazima tuendelee kutoa ibada.
Waumini wa Kanisa la Mungu hushika ibada zote
kama vile siku ya Sabato na Pasaka,
na wanaelekea msamaha wa dhambi
na tumaini la Mbinguni ambalo Mungu Ametuahidi.
. . . akawa chanzo cha wokovu wa milele kwa wote wanaomtii.
Naye amewekwa na Mungu kuwa Kuhani Mkuu kwa mfano wa Melkizedeki. Waebrania 5:9–10
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha